Breaking News

Your Ad Spot

Sunday, October 29, 2023

MWANDISHI ALIPOPIGWA KIKUMBO KATIKA HEKAHEKA ZA MAPOKEZI YA MAKONDA DAR

Na Bashir Nkoromo, Wazalendo Blog
Katibu mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Paul Makonda, baada ya kuteuliwa na CCM kushika nafasi hiyo, alipokewa rasmi jijini Dar es Salaam, Octoba 26, 2023.

Kwa jumla alipokewa kwa shamrashamra na hekaheka za inayoweza kutajwa kuwa ilikuwa ya kiwango cha juu mno katika mapokezi wenye hayo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba na baadaye kwenye viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam.

Katika hekaheka hizo yapo mengi yaliyojiri, lakini kuna tukio nililiona na kupigapicha ambalo licha ya furaha niliyokuwa nayo katika kushiriki mapokezi hayo, lakini linistua ni la mwandishi wa chombo kimoja cha habari kupigwa kikumbo hadi kugaragara chini!

Mbali na kustushwa na tukio hili, pia linifanya kuwaza mbali kuhusu hatma ya usalama wa mwandishi/mpigapicha wa habari anapokuwa kazini, hasa katika matukio makubwa kama hili linalomlazimu awe karibu mno na tukio ili apata picha na sauti kwa vizuri.

Natanguliza kuomba radhi na msamaha wa bure kwa mwandishi mhusika na kwa yeyote atakayemgusa visivyo, silitangazi tukio hili kwa lengo la kudhihaki au kudhalilisha, ila kuelimisha tu. 



Picha: Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages